Xlestrade walifanya mkutano na Patrizia Gualandi na Mauro Raggioli ambao ni wasimamizi na wanachama wa Karibuni Onlus Bologna.
Offisi kuu za shirika zipo San Lazzaro of Savena (Bologna). Wazo la shirika hili lilizaliwa mwaka wa 1989 kusudi ya safari ya wasichana wawili kule Tanzania kuzuru rafiki yao.
Katika safari yao mawazo yao yalitekwa na lile jumba la watoto yatima huko Mgolole, karibu na Morogoro, yapata 200km kutoka Dar es Salam, inayoendeshwa na kikundi cha watawa wa Tanzania. Tangu hiyo siku wasichana hao waliamua kulifadhili hilo mradi.
Uchaguzi wa neno “Karibuni” kama salamu, inalengo la kukaribisha kila mtu ambaye angependa kukaribia shughuli za hili shirika.