Contact Person: Andreina Iorio, Cleopas Wachira; Telephone Number: +254 713918716;
E-mail: thenanyukifurahafoundation@gmail.com
Website: www.thenanyukifurahafoundation.weebly.com.
Tulifanya mkutano na Andreina Iorio, mmoja wapo wa waanzilishi wa The Nanyuki Furaha Foundation mwaka wa 2014 pamoja na Cleopas Wachira. Shirika lao lipo Kenya katika mji wa Nanyuki.
Andreina na Cleopas walianza kazi yao mwaka wa 2013 ndani ya jumba la watoto wa mtaani uliokuwa chini ya serikali ya ndani mjini Nanyuki.
Walitueleza kwamba jumba lile halikuwa likiendeshwa kwa utaratibu mwafaka. Hilo ndilo sababu la wao kufanya uamuzi wa kuwakaribisha watoto wale nyumbani kwao.
Furaha ndio mwongozo wa “The Nanyuki Furaha Foundation” ndivyo walivyobuni jina la shirika.
Walianza na nia ya kuwaokoa watoto wa mtaani, watoto walemavu na yatima. Lengo kuu ni kuwarekebisha na kuwarejesha watoto katika familia zao. Kwa miaka za mwanzo The Nanyuki Furaha Foundation ilitegemea mashirika za Italia ilikupata raslimali na mahali ya kuwaweka watoto. Kutoka Desemba 2014 hadi Mai 2015 walitetemea jumba la Africa Milele Onlus lakini wamekuwa wakishirikiana na Col cuore per l’ Africa Onlus kutoka Mondovì (CN).
Kwa wakati huu shirika linaendeshwa ndani ya jengo lililo kuwa shule pamoja na shamba ambayo mapato yake ni ya mradi kujimudu. Hadi sasa watoto walioko pale ni 40, na kila mmoja na historia yake ya uchungu kueleza.
The Nanyuki Furaha Foundation inaelekea kufikia kiwango cha shirika lisilo la serikali(NGO) kutoka kwa serikali ndongo hivi Karibuni. Lengo yao ya siku za usoni ni kununua ardhi na kujenga jumba mpya la watoto, maabara vyumba vya mikutano na darasa za ‘vocational skills’.
Hapa Italia shirika hili linategemea Col cuore per l’ Africa Onlus na bado hawana mipangilio au shughuli za kuchangisha fedha. Hata hivyo kunauwezekano kuwasiliana na The Nanyuki Furaha Foundation ilikuanza kujitolea kikazi kwenye mradi kule Kenya. Wanafunzi wa chuo kikuu cha udaktari wananafasi ya kufanya “internship” kule Kenya.
Xlestrade iliwauliza neno moja ambayo wanaweza kutuachia. Andreina alitiliamkazo kuwa The Nanyuki Furaha Foudation siyotujumba la watoto bali ni familia kamili, na ni wazi kwa mtu yeyote ambaye angependa kuwasiliana nao.
Tungependa kumshukuru Andreina kwa kuwasiliana nasi ilikutueleza motisha na Furaha yake, hata kama kuna changa moto chungu nzima. Tunawatakia safari njema yenye maendeleo mengi tukitumai tutafanya kwa pamoja!
Traduzione a cura degli amici kenyoti di Maralal